Vikosi vya usalama vya Burkina Faso vimesema, zaidi ya wanawake 60, wakiwemo watoto na wasichana waliotekwa nyara wiki iliyopita na watu wanaoshukiwa kuwa ni wanajihadi kaskazini mwa nchi hiyo wameachiliwa huru.

Tukio hilo limetokea baada ya Vikosi hivyo vya usalama kuendesha oparesheni ya uokoaji wa kundi hilo la watu na kuwapata wanawake 27 watoto na wasichana wapatao 39, jirani na jimbo la kati ya Kaskazini.

Akina mama na watoto wakiendelea na maisha ya kawaida nchini Burkina Faso. Picha ya The Guardian.

Wahanga hao, walitekwa nyara wakiwa katika shughuli za utafutaji matunda pori na vyakula vingine ambapo idadi yao iliozidi kupanda na kufikia watu karibu 80 na hivyo kuzua taharuki huku Maafisa wa Umoja wa Mataifa wakitaka watu hao waachiliwe bila masharti.

Tukio la utekaji nyara wa idadi kubwa ya watu nchini humo, halijawahi kushuhudiwa licha ya taifa hilo la Afrika Magharibi kukabiliwa na uasi uliokithiri wa itikadi kali uliofungamana na makundi ya dola la kiislam na Al-Qaeda tangu mwaka 2015.

Robertinho: Hakuna kama Mgunda, Matola
Prince Dube: Hatutakuwa wanyonge tena