Watu wanne familia moja wamefariki dunia kwa kuteketea na moto baada ya baba wa familia hiyo, Aman Madumba (72), kujifungia chumbani na watoto hao kisha kuchoma nyumba moto.

Familia hiyo ya kijijini Malolo B kilichopo Wilayani Kilosa mkoani Morogoro inajumuisha Baba huyo na watoto wake watatu ambao ni Habibu Aman (10), Sadick Aman (8) wote wa darasa la tatu na Bahati Aman (5), ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha tatizo.

Awali, akisimulia tukio hilo mjukuu wa marehemu, Mwanjaa Madumba amesema majira ya saa saba usiku wa kuamkia Mei 5, 2023 akiwa amelala aliona moshi mkubwa chumbani kwake na alipotoka aligundua ulikuwa ukitokea upande wa chumba cha babu yake.

“Nilipiga kelele Watu wakafika na kuzima moto huo na walipofungua mlango wa chumbani walikuta wote wanne wameteketea na moto,” alisimulia mjukuu huyo huku ikidaiwa huenda msongo wa mawazo umesababisha hali hiyo kwani marehemu huyo alitengena na mkewe.

Uongozi PSG yalaani vitendo vya Mashabiki
Lewandowski, Benzema wafukuzana Kiatu cha dhahabu La Liga