Mkuu wa shirika la haki za binaadamu, Volker Turk amesema ameshangazwa na juhudi za utaratibu wa kuwanyang’anya wanawake haki zao, huku akibainisha kuwa hali hiyo haitafanikiwa.
Turk, ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na wanahabari na kuongeza kuwa unyanyasaji wa wanawake mitandaoni umekuwa ukienea katika mataifa mengi ulimwenguni ikiwemo nchini Afghanistan na Iran.
Amesema, ili kuipinga hali hiyo, anatazamia kuzuru miji ya Kabul na Tehran kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na maafisa wa maeneo hayo kwani hali iliyopo Afghanistan ni mbaya.
Aidha amefafanua kuwa, suala hilo linatia wasiwasi kwani takribani miaka 75 baada ya Azimio la Kimataifa la Haki za Binaadamu kupitishwa, juhudi za kuwanyima haki wanawake na wasichana zinaongezeka.