Mwanasiasa mkongwe nchini, Steven Wasira ametoboa siri ya ushindi ya kupata kura nyingi mara mbili mfululizo katika uchaguzi wa Halmashauri kuu ya CCM (NEC).

Amesema kuwa kuwa kuongoza kwake katika uchaguzi huo mkubwa wa Chama cha Mapinduzi CCM ni ishara kubwa kwamba wanachama wenzake wanamkubali kwa asilimia zote.

“Wakati wa mchakato wa Katiba mpya, CCM ilikuwa na msimamo wa serikali mbili, tuliamini kuwa ili kuwe na muungano imara ni lazima kuwe na serikali mbili na hata mimi msimamo wangu ulikuwa hivyo hivyo,  hii ni moja ya vitu ambavyo vimekuwa vikinitengezea mazingira mazuri katika siasa,”amesema Wasira

Amesema kuwa kipindi hicho CCM ilikuwa na msimamo wa serikali mbili ambapo kwa kiasi kikubwa aliweza kushiriki katika mijadala mbalimbali ya Mabadiliko ya katiba.

Hata hivyo, Wasira ameongeza kuwa kitu kikubwa kilichombeba katika uchaguzi mkuu wa CCM ni misimamo yake ya kukipigania chama na kuwa imara.

 

Nandy akata kiu ya mashabiki wa Video ya Kivuruge, itazame
Polisi wavamia shule ya Kiislamu