Watu sita wameuawa  na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa baada ya watu wenye silaha kushambulia mabasi mawili eneo la Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.

Vyombo vya habari nchini humo vinasema watu wawili walifyatulia risasi mabasi hayo yaliyokuwa kwenye msafara.

Mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi ameripoti taarifa ya shambulio hilo kuwa limetokea siku moja tu baada ya Marekani kutoa tahadhari mpya kwa raia wake kuhusu usalama baadhi ya maeneo ya Kenya.

Aidha inasemekana kuwa Serikali ya Kenya ilikuwa imetahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mashambulio ya kigaidi huku mfungo wa mwezi wa Ramadhan ukikaribia kumalizika.

Kamati ya usalama katika jimbo la Mandera ilikuwa pia imewaonya watu wasio wa asili ya Kisomali dhidi ya kusafiri eneo hilo kwa kutumia barabara wiki hii.

Shambulio hilo la ijumaa ndilo la tatu kutekelezwa kwenye mabasi ya uchukuzi wa umma Mandera.

Video: Rais wa Rwanda Paul Kagame azungumzia uhusiano wa Tanzania na Rwanda
Ronaldo de Lima Aeleza Hisia Zake Kuhusu Lionel Messi