Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbarawa, anatarajiwa kuzindua wiki ya usalama wa reli nchini iliyoanza Ctobar 9 hadi hadi Oktoba 16 mwaka huu
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Habibu Suluo imewataka watumiaji wa huduma za reli na wananchi kuwa waangalifu wanapotumia huduma za reli.
Amewataka kuchukua tahadhari za kiusalama wakati wote wanaotumia huduma za reli wakiwa kwenye vituo vya reli ndani ya mabehewa na wanapopita kwenye maeneo ya reli.
”Ni muhimu kufahamu kuwa tren zinapita kwa mwendo kasi na zinaweza kukawia kushindwa kusimama ghafla inapotokea dharura, hivyo basi ni wajibu wa kila mwananchi kuchukua tahadhari ili kuokoa maisha” amesema Suluo.
Imeelezwa kuwa Shirika la reli Tanzania (TRC) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Reli ya Tanzania Zambia TAZARA watahakikisha kuw ahuduma za usafiri wa reli nchini zinatolewa kwa ubora na usalama kwa watumiaji na wananchi kwa ujumla.
Aidha LATRA imewataka wananchi kuunga mkono juhudu za Serikali katika uwekezaji mkubwa unaondelea ili kuboresha miundombinu ya reli na kukuza uchumi wa tanzania.
Maadhimisho ya wiki ya usalama wa reli mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo Chukua Tahadhari Treni zinamwendo wa haraka ni hatari.