Wafanyakazi wawili wa kiwanda cha sukari Mtibwa kilichopo Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro waliofahamika kwa majina ya Hamis Said (29), na Frank Kennedy (26), wote wakiwa ni wakazi wa Dakawa Wilayani humo wamefariki baada ya kutokea mlipuko kiwandani hapo.

Tukio hilo limetokea Aprili 12, 2023 katika eneo la kiwanda hicho ambapo Kaimu Afisa Uhusiano Hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro, Scolastica Ndunga amekiri kupokea miili ya Watu wawili na kusema miili yao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti huku majeruhi wakilazwa hospitali iliyopo ndani ya Kiwanda hicho.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro, Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema hadi sasa bado haijaifahamika sababu za mlipuko huo na uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea.

DCEA, TAKUKURU kushirikiana mapambano dawa za kulevya, rushwa
Sudan, Tanzania, Rwanda zavutana Kagame Cup 2023