Johansen Buberwa – Kagera.

Watu wawili wamehukumiwa kifo huku wengine watano wakihukumiwa kwenda jela miaka thelathalini, baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha na makosa ya unyanyasi wa kijinsia.

Akizungumza na Vyombo vya Habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Blasius Zablon Chatanda amesema hatua hiyo inafuatia juhudi za Polisi katika kupambana na kudhibiti matukio ya uhalifu.

Katika tukio jiingine Kamanda Chatanda amesema jumla ya pikipiki 65 zilikamatwa Wilaya za mkoani humo kutokana na kuhusika katika matukio mbalimbali ya uhalifu.

Amesema, pia watuhumiwa 14 waliokuwa wakijihusisha na utekaji wamekamatwa huku watuhumiwa wengine 11 wakikamatwa kwa kujihusisha na wizi mifugo katika maeneo mbalimbali.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 15, 2023
Young Africans kushusha vyuma Dirisha Dogo