Wazazi na Walezi nchini, wametakiwa kuwalinda watoto wao kama wanavyolinda mali nyingine ili kuwaepusha dhidi ya matukio mbalimbali ikiwemo kufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo ubakaji na ulawiti.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum, Dkt. Dorothy Gwajima hii leo Juni 3, 2023 wakati akizindua Kampeni ya ‘‘Sema Nao’’ iliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa lengo la kuelimisha Jamii kamasuala ya kiuhalifu na ukatili wa Kijinsia.

Katika uzinduzi huo, Waziri Gwajima pia amewataka watoto kukataa zawadi wanazopewa na watu wasiowafahamu ama wanapoitwa na watu wasiowafahamu kutokana na mbinu hizo hutumiwa na watu wabaya na kuwarubuni.

Kampeni hiyo imezinduliwa katika viwanja vya Shule ya Msingi Ihumwa Jijini Dodoma, na kuhudhuriwa na wanafunzi, viongozi wa Serikali, wananchi pamoja na Maafisa toka Jeshi la Polisi.

Hawa watatu wanapigwa bei FC Bayern Munich
Madai ya kuandika Biblia yake, Polisi wamhoji Nabii Yohana