Shangwe na nderemo vilitawala katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare na kwingineko nchini humo mara tu baada ya Spika wa Bunge, Jacob Mudenda kuisoma barua ya Rais Robert Mugabe kujiuzulu wadhifa wa rais kwa hiari yake.
Tangazo hilo la kushtukiza lilisomwa katika kikao maalumu cha bunge na seneti, ambacho kilikuwa kimeanza mchakato wa kisheria ambao hatimaye ungemng’oa Mugabe madarakani,
Aidha, Mugabe alisema katika barua yake ya kujiuzulu kuwa amefanya hivyo kwa kuzingatia maslahi ya taifa, na kuwapa nafasi watu wengine ili waweze kuiongoza nchi hiyo katika nyanja tofauti tofauti.
Rais Mugabe alimfukuza kazi makamu wake wa Rais, Emmarson Mnangagwa wiki mbili zilizopita, hatua ambayo ilichukuliwa na wanaharakati mbalimbali kama kumtengenezea njia mkewe Grace kuwa mrithi wa kiti cha urais.
-
Odinga: Hatuitambui serikali ya Uhuru Keyatta
-
Mugabe akutanishwa na hasimu wake aliyemtimua
-
Mnangagwa amkomalia Rais Mugabe ajiuzulu
Hata hivyo, Jeshi la nchi hiyo limehimiza utulivu na kuheshimu sheria wakati wa shamra shamra zinazoendelea, huku Kamanda Mkuu, Constantino Chiwenga amesema kuwa vitendo vyovyote vya fujo na ulipaji kisasi vitakabiliana na mkono mkali wa vyombo vya usalama.