Hatimaye Waziri wa Mipango nchini Kenya, Anne Waiguru aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma nzito za ufisadi ameamua kujiuzulu.

Waiguru ambaye ripoti za ukaguzi wa manunuzi ya umma zilionesha kuwa alinunua kalamu moja kwa dola 100 (zaidi ya shilingi 200,000 za Tanzania) kwa ajili ya ofisi yake, amewaambia waandishi wa habari kuwa amemuandikia rais Uhuru Kenyatta barua ya kujiuzulu kwenye nafasi hiyo baada ya kushauriwa na daktari wake.

Alisema kuwa daktari wake alimshauri aachie nafasi hiyo kutokana na kushambuliwa na maneno ya kashfa ya ufisadi kila kona hali iliyomuathiri kisaikolojia.

“Familia yangu iliathirika mno kwa mashambulizi kutoka kwa watu ambao walitaka niondoke kutoka wizara hii,” alisema huku akikanusha vibaya tuhuma hizo za ufisadi.

Mbali na kalamu, waiguru anakabiliwa na tuhuma za kununua runninga ya ofisini kwake kwa $19,000, Kompyuta mpakao kwa s$11,000, zulia la ofisi yake kwa $3,800, program ya kulinda computer (antivirus) kwa $9,737 na program ya kompyuta ya Adobe kwa $19,000.

Wazanzibar Waandamana Ikulu ya Marekani Kuhusu Mgogoro wa Zanzibar
Kufutwa Sherehe Za Uhuru 'Disemba 9' Mwisho Uko Hapa...