Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametaka ndani ya saa 48 Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzanite awe amekamatwa kutokana na tuhuma zinazomkabili za kudhulumu Fedha za Wakulima wa zao la Parachichi wa Wilaya ya Tukuyu Mkoani Mbeya.

Bashe ametoa agizo hilo hii leo Agosti 7, 2022 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na kusema Kampuni hiyo pia iliondoka salio la zaidi ya Shilingi Milioni 30, ambazo ni fedha za Wakulima wa zao la Parachichi Wilayani Rungwe.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Amesema, “Kampuni hiyo ilichukua fedha za Wakulima zipatazo milioni 138 na hadi sasa imerejesha shilingi milioni 100 tu sasa nawataka kukamilisha malipo hayo yaliyosalia haraka.”

Waziri Bashe amebainisha kuwa, Serikali haitaki kuona sekta Binafsi zikiwadhulumu Wakulima mazao yao, na kuongeza kuwa wanapaswa kuheshimu na kuthamini jasho na gharama walizotumia Wakulima.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 08, 2022
Rais na Rais mstaafu wamaliza tofauti zao