Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amewapokea na kufanya mazungumzo na wajumbe kutoka nchini Brazil ambao wako katika ziara ya kwenda kutembelea Chuo cha Michezo Malya Jijini Mwanza kwa ajili ya shughuli za kuendeleza michezo.
Wajumbe hao ambao ni Ndugu Paulo Pan kutoka International Promotion Through Sports na Flavio Pazeto kutoka Ubalozi wa Brazil nchini wamefika Jijini Dodoma Juni 23 2021
Katika mazungumzo hayo Mhe. Bashungwa amemshukuru Balozi wa Brazil nchini Mhe. Antonio Augusto Cesar na Serikali yao kwa kuitikia wito wa kikao cha Mei 21 2021 Jijini Dar es Salaam kilichokuwa na ajenda ya kushirikiana katika sekta maendeleo ya michezo nchini hasa katika upande wa soka na mchezo wa masubwi kwa kufanya Programu ya kubadilishana wakufunzi.
“Tumekubaliana kuanzisha ushirikiano na Paulo Pan kutoka International Promotion through Sports katika kuendeleza sekta ya michezo nchini” amesema Mhe.Bashungwa.
Makubaliano hayo ambayo Wizara na International promotion Through Sports yatafikiwa yatatoa fursa kujadili uwezekano wa kukutana na Kamati ya Olimpik ya Dunia na Shirika la UNESCO kuhusu namna ya kutunisha Mfuko wa Maendeleo wa Michezo nchini.