Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amekuwa mtanzania wa kwanza kunywa dawa ya kufubaza virusi vya corona ambayo imetengenezwa visiwani madagascar.

Waziri kabudi amekunywa dawa hiyo baada ya kuwasili nchini madagascar kupokea msaada wa dawa na kupokelewa na Waziri wa mambo ya nje wa Madagascar Mhe. Tehindrazanarivelo Djacoba As Oliva.

Dawa hiyo inahusishwa na mmea wa Kichina unaoitwa Artemisia (pakanga) – ambao ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria.

Mume wa Mwimbaji Jennifer Mgendi afariki dunia

Ikumbukwe kuwa Marais wa Tanzania, Jamuhuri ya Congo, Guinea Bissau na Equatorial Guinea wote wamemaua kutuma ndege nchini Madagascar kuchukua dawa hiyo ya mitishamba ili kuwapa wananchi wao.

Ujumbe wa mwisho wa marehemu OCCID Masoud "Allah atujalie mwisho mwema''
Mume wa Mwimbaji Jennifer Mgendi afariki dunia