Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa amewasilisha Bungeni maelezo ya awali kuhusu mapendekezo ya kuridhia mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa Bandari nchini.
Prof. Mbarawa amewasilisha maelezo hayo hii leo Juni 10, 2023 na kuzityaja changamoto mbalimbali za kuchukua hatua mbalimbali za maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, bado ufanisi katika utoaji huduma za bandari haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.
Amesema, hali ya sasa ya utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na bandari shindani kikandaakitoa mfano wa wastani wa meli kusubiri nangani kwa Bandari ya Dar es Salaam ni siku 5 ikilinganishwa na siku 1.25 kwa Bandari ya Mombasa na siku 1.6 kwa Bandari ya Durban.
Prof. Mbarawa ameongeza kuwa, ufanisi mdogo wa Bandari ya Dar es Salaam umetokana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kukosekana kwa mifumo ya kisasa ya TEHAMA, kutokuwepo kwa
maeneo ya kutosha ndani na nje ya bandari kwa ajili ya kuhifadhia shehena.
Mpungufu mengine ni pamoja na maegesho ya meli na kukosekana kwa mitambo ya kutosha na ya kisasa ya kuhudumia shehena ambayo teknolojia yake inabadilika mara kwa mara na ina gharama kubwa ya uwekezaji na uendeshaji.