Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo kuanzisha Mamlaka ya Kilimo cha Mazao ya Bustani na Kituo cha Utafiti kwa ajili ya kusimamia na kuratibu mazao yamatunda, viungo na mboga. Hii ni kutokana na umuhimu wa tasnia ya kilimo cha mazao ya bustani ,
Majaliwa alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kikanda la Biashara la Uwekezaji katika Tasnia ya Mazao ya Bustani lililofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, jijiji Dar esSalaam
Amesema tasnia ya kilimo cha mazao ya bustani ina mchango mkubwa kwenye maendeleo ya uchumi nchini na inauwezo wa kutoa ajira za watu zaidi ya milioni nne, hivyo kuongeza kipato kwa wakulimana wafanyabiashara.
“Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita uzalishaji wa mazao ya bustani uliongezeka kwa asilimia 10.5 kutoka tani 5,931,900 mwaka 2015/16 hadi 6,556,102 mwaka 2018/19” amesema Majaliwa.
Waziri Mkuu amesema kuwa mbali na kuchangia katika ukuaji wa uchumi,tasnia hiyo itasaidia kujenga taifa la watu wenye afya nzuri, nguvu na uwezo wa kufanya kazi.
Aidha amesema kuwa mazao ya bustani yamekuwa na mchango mkubwa katika kupambana na Corona kwa sababu dawa mbadala za asili zilizosaidia wananchi wengi duniani kote kudhibiti ugonjwa huo zilizotokana na matunda na vioungo.