Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida amenusurika na kuondolewa bila kujeruhiwa kwenye tukio la hadhara baada ya kile kilichoonekana kuwa ni bomu la moshi kurushwa jirani na eneo alilokuwa akitoa hotuba huko Wakayama.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya Habari, vimeseoa tukio hilo limetokea hii leo Aprili 15, 2023 na kwamba Waziri Mkuu huyo hajapata madhara yoyote na tayari mtu mmoja amekamatwa katika eneo la tukio akishukiwa kutekeleza shambulio hilo.
Shuhuda mmoja alisema waliona mtu akirusha kitu, na baadaye kufuatiwa na moshi, huku mwingine akisema walisikia kishindo kikubwa ingawa hakukuwa na majeraha yaliyoripotiwa huku mtuhumiwa akitambuliwa na mamlaka kama Ryuji Kimura (24).
Shirika la utangazaji la umma la Japan, NHK, lilimnukuu Kishida akisema kulikuwa na “mlipuko mkubwa” kwenye ukumbi huo. “Polisi wanachunguza maelezo, lakini ningependa kuomba radhi kwa kuwatia wasiwasi watu wengi na kuwasababishia matatizo.”