Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba ameagiza kikosi maalum cha Jeshi la Polisi kuwasaka walimu wa kiume wanaoonekana kwenye kipande cha video mtandaoni wakimuadhibu kikatili mwanafunzi.

Kipande hicho cha video ambacho bado hakijajulikana kimechukuliwa katika shule gani kinawaonesha walimu kadhaa wa kiume wa kumshambulia mwanafunzi kwa fimbo na makofi makali ya usoni ndani ya chumba cha darasa ama ofisi ya walimu.

Wakati adhabu hiyo kali ikiendelea, inasikika sauti ya Mwalimu wa kike ambaye anawasihi walimu hao kusitisha adhabu hiyo, “mtamuumiza jamani” .

Waziri Nchemba ameonesha kusikitishwa na tukio hilo na amewataja walimu hao kama majambazi.

“This is real sad. Nimewatuma watu wa mtandao walocate tukio lilipotokea na kuwakamata hao majambazi. Maana mwalimu hawezi kuwa na ukatili wa kijambazi namna hiyo, “ameandika Waziri Nchemba.

Naye Waziri wa Elimu, Joyce Ndalichako ameonesha kusikitishwa na tukio hilo na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili walimu hao waweze kukamatwa na kukumbana na mkono wa sheria.

Simba SC Waitaka Radhi Serikali Ya John Pombe Magufuli
Zitto Kabwe - Sasa hivi mabomu yanalipuliwa na mkuu wa nchi mwenyewe