KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, ametajwa kuwa kocha bora wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mwezi Oktoba.

Wenger amepata tuzo hiyo baada ya mwezi huo kwenda vizuri kwake kwa kuanza na ushindi dhidi ya Manchester United, wa bao 3-0 kwenye dimba lao la nyumbani, Emirates Stadium.

Ushindi mwingine tena dhidi ya Watford, Everton na Swansea City ulimsaidia kufikia pointi sawa na Manchester City FC inayoongoza Ligi hiyo.

Hii ni ni tuzo ya 15 ya mwezi kwa Wenger tokea atue Arsenal mwaka 1996 akitokea Grampus Eight ya Japan.

Mavuno ya Pamba Yaongezeka, Wakulima Wasubiri Viwanda Vya Magufuli
Taifa Stars Kurejea Nyumbani Kesho