Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ameingilia kati sakata la kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Sam Allardyce ambaye anakabiliwa na tuhuma za kufichua siri za waajiri wake (Chama cha soka nchini humo FA).

Wenger amesema Allardyce kupewa fursa ya kujitetea dhidi ya madai yaliyoibuliwa na gazeti la Daily Telegraph.

Uchunguzi wa gazeti hilo umeeleza kuwa Allardyce mwenye umri wa miaka 61,alitumia cheo chake kushauri mpango wa pauni 400,000 na kutoa ushawishi wa kuweza ”kuzunguka” sheria za uhamiaji wa wachezaji.

Allardyce ambaye aliwahi kuvinoa vikozi vya klabu za Bolton,Newcastle na West Ham pia amelikosoa shirikisho la soka nchini Uingereza FA, aliyemrithi Roy Hodgson, na aliyekuwa naibu wake Gary Neville.

”Ni muhimu kumwacha Allardyce kujitetea na ninatumai atasafisha jina lake”,alisema Wenger.

Allardyce bado hajajibu madai hayo, na tayari ameshakutana na mwenyekiti wa FA Greg Clarke na afisa mkuu wa shirikisho hilo Martin Glenn.

Video: Makonda ahitimisha zoezi la upimaji afya Jijini Dar es salaam
TFF Yatangaza Viingilio Vya Mpambano Wa Young Africans Vs Simba