Watu wanne wamethibitishwa kufariki eneo la Taita Taveta, baada ya mafuriko kuikumba mitaa mbalimbali ya mji wa Voi Nchini Kenya na viunga vyake.

Aidha, inaarifiwa kuwa hivi punde mwili wa mama mmoja umepatikana kando mwa mto huo huku miili ya wanaume watatu ikipatikana katika mto, Voi ambao kwa sasa umefurika maji.