Mpinzani na mgombea Urais Delly Sesanga amejiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho katika Uchaguzi Mkuu nchini DRC na kutangaza kumuunga mkono Moïse Katumbi, gavana wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Kinshasa Delly Sesanga amehalalisha chaguo lake kwa kuongeza bahati kwa upande wa upinzani kwa lengo la kumtimua mamlakani Félix Tshisekedi kupitia sanduku ya kura.

“Hii ni kuongeza nafasi ya upinzani ya kuwa na mbadala katika nchi hii. Hii sio chaguo lililofanywa na mtu mmoja. Ni chaguo kuhusiana na mradi wa pamoja ambao tumeunda kwa kuunganisha mapendekezo yetu yote. Pia ni kuhusu uwezekano kwamba kuna, leo, kuunda kambi, muungano ambao unaweza kutoa mtazamo mpya kwa nchi hii na nchi inauhitaji.

Mwanasiasa wa upinzani na mgombea Delly Sesanga

“Kutokana na kushindwa dhahiri kwa utawala wa Tshisekedi anaye maliza muda wake, tunahitaji kwenda zaidi ya kila mmoja kupendekeza kitu tofauti na ndicho tunachofanya. Na mijadala hii lazima iendelee na kila mtu mwingine ambaye anadhani kwamba kuna haja ya kuwa na njia mbadala katika nchi hii.

“Pia tutatoa ulinzi na kujihusisha, kwa makubaliano ya pande zote, na ufuatiliaji wa uchaguzi, kwamba matokeo ya uchaguzi, kituo cha kupigia kura kwa kituo cha kupigia kura, yataheshimiwa. Wananchi lazima wahamasishwe siku moja kuokoa miaka mitano ya maisha yao na hivyo ni dhabihu ya lazima na ya jamhuri,” amesema Delly Sesanga.

Takribani wagombea 26 walitangaza kuwania nafasi ya Urais, wamesalia 22 baada ya wagombea 4 akiwemo Waziri Mkuu wa zamani Matata Poyo kujitokeza nyuma ya Moïse Katumbi.

Rais anayemaliza muda wake Félix Tshisekedi ni mgombea kwenye kinyang’anyiro cha urais kwa muhula wa pili wa miaka mitano.

Wengine wanne wafariki kwa mafuriko
Kipindupindu Kagera: Wanne wafariki, uchunguzi waanza