Johansen Buberwa – Kagera.

Watu wanne wamefariki kwa ugonjwa wa Kipindupindu katika Kijiji cha Buchurago kilichopo Kata ya Bugorora Wilayani Misenyi, huku wengine wanne wakilazwa Hospitali ya St. Tereza kwa matibabu na watatu wakiruhusiwa.

Akizungumza na vyombo vya Habari hii leo Desemba 4, 2023, Mkuu wa Mkoa Kagera Hajath Fatma Mwasa amesema Serikali inaendelea na uchunguzi kwa watu wote walio tangamana na tayari imechukua sampuli 18 za ugonjwa huo uliotokea Novemba 29, 2023.

Amesema, “Ugonjwa huu ni hatari sana na inatakiwa kuendelea kuchukua taadhari maana unaenea kwa kasi sana na ni lazima kuwa waangalifu kwa kufuata maelelezo sahihi ya wataalamu na kujielekeza katika mbinu za usafi wa mazingira.”

Hata hivyo, Katika hatua nyingine amewataka wakazi wa Mkoa huo kuacha mikusanyiko, kutokula chakula kwenye mikusanyiko na kunawa mikono mara kwa mara.

Uchaguzi DRC: Wanaomuunga mkono Katumbi waongezeka
Rais TFF apongezwa kwa utendaji