Mbunge mmoja nchini Kenya ametakiwa kuomba radhi mara baada ya kutuma ujumbe wa kimapenzi kwenye group la Whatsapp la wabunge.
Anthony Kiai alituma ujumbe wa kimapenzi kwenye group na kuwaomba wabunge wenzake kutoutilia maanani kwani amekosea lakini wabunge wenzie katika group hilo walimtaka kuomba radhi.
Aidha, Admin wa group hilo, Bernad Chege, alimuomba mbunge huyo kuomba radhi, na badala yake msaidizi wa Mbunge huyo ndio akaomba radhi kwa kitendo hicho cha bosi wake kutuma ujumbe wa mapenzi katika group hilo
Ujumbe huo ulioandikwa kwa lugha ya Gikuyu ambayo inaongelewa na Wakikuyu nchini Kenya, ilikuwa ikitoa maelezo jinsi ya kumridhisha mwanamke chumbani, huku baadhi ya wabunge wengine walionekana kumtetea wakisema ngono sio dhambi.
-
Uchaguzi Liberia kuelekea duru ya pili
-
Mwandishi nguli wa habari za uchunguzi auawa
-
Diana Rwigara ataka familia yake kufutiwa mashtaka
Hata hivyo, Mbunge Kiai amekuwa mbunge wa jimbo la Mukurweini kufuatia ushindi alioupata kwenye uchaguzi wa Agosti 8, 2017