Mwandishi maarufu wa habari za uchunguzi katika visiwa vya Malta ameuawa wakati gari alilokuwa akiliendesha kulipuliwa na bomu visiwani humo.

Daphne Caruana Galizia ambaye alikuwa mwandishi nguli nchini humo, alikuwa akiitumia blogu yake kuandika taarifa zinazohusu kesi za madai ya rushwa zikiwemo za wanasiasa visiwani humo.

Aidha, wakati wa uhai wake, Dphine alikuwa akimshutumu waziri mkuu wa visiwa hivyo, Joseph Muscat, na mkewe kutumia akaunti za benki za siri ili kuficha malipo kutoka kwa familia ya utawala wa Azerbaijan suala ambalo waziri mkuu na familia yake wamelikana.

Hata hivyo, kwa upande wake waziri mkuu wa visiwa hivyo, Muscat amelaani mauaji hayo ambayo ameyaita ni ya kinyama, hivyo na kuahidi kuhakikisha wanakamatwa wote waliotekeleza mauaji hayo.

Video: Lissu anyanyuka, Watanzania wanaokamatwa China madawa wafyekwa
Diana Rwigara ataka familia yake kufutiwa mashtaka