Mkurugenzi Mtendaji wa Programu za Dharura za Afya kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Mike Ryan amesema virusi vya corona vinaweza vikaendelea kuwepo na kujiunga na mchanganyiko wa virusi vingine vinavyoendelea kuua watu duniani.
Dkt.Ryan ametolea mfano virusi vya UKIMWI ambavyo hadi leo vipo akisema hafananishi virusi hivyo ila ni vyema Watu kujua uhalisia, kwa kuwa hakuna anayeweza kutabiri siku ambayo covid 19 inaweza kuondoka.
Amesema kuwa chanjo inaweza kupunguza madhara ya virusi vya corona, lakini chanjo inapaswa kuwepo na kuwa na ufanisi wa hali ya juu na kupatikana kwa kila mtu duniani.
“Ni muhimu kufahamu Virusi vinaweza kuwa janga jingine katika jamii zetu, na virusi hivi huenda visiishe ,” amesema Dkt Ryan akiwaambia waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Geneva.
Mpaka hivi sasa takribani watu 300,000 kote duniani wameripotiwa kufa kutokana na virusi vya corona, na zaidi ya visa milioni 4.3 vimerekodiwa.
Madereva 23 wa Tanzania wazuiwa kuingia Kenya baada ya kukutwa na virusi vya corona
Waumini 44 wa parokia moja wafariki kwa corona, mchungaji aeleza