Shirika la afya duniani WHO limeonya kuwa mataifa tajiri hayapaswi kutumia nyongeza ya chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 kama suluhisho la kudumu dhidi ya janga la virusi vya Corona.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo la WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema matumizi ya nyongeza ya chanjo huenda yakarefusha muda wa janga hilo la virusi vya Corona badala ya kulimaliza kabisa.

Ghebreyesus pia ametahadharisha kuwa sherehe za mkesha wa mwaka mpya zitakazofanywa kiholela bila ya kuzingatia masharti ya afya zinaweza kuwa chanzo cha maambukizo mapya.

Hayo yanaarifiwa wakati Ufaransa imekuwa moja kati ya mataifa ya kwanza duniani kuanza kutoa chanjo kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 5 hadi 11, huku Uingereza pia ikiidhinisha chanjo ya Pfizer kwa watoto.

Mwenendo wa FC Barcelona wamsikitisha Xavi
Nketiah afunguka ushindi wa Arsenal