Siku tatu baada ya klabu ya Chelsea ya Uingereza kumtimua kocha Jose Mourinho, mashabiki mbalimbali wa soka nchini Tanzania wameandika nyimbo za utani juu ya Mreno huyo mwenye maneno mengi.

Mashabiki hao wamekopi baadhi ya mistari ya wimbo wa ‘Je Utanipenda’ wa mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond Platinum.

Wimbo huo umeonekana kutamba muda mfupi tangu uingie sokoni siku chache zilizopita.

Katika wimbo huo Diamond alikuwa akijaribu kuhoji kile ambacho kitamtokea endapo ikitokea bahati mbaya akafilisika.

Lakini mashabiki wa soka wakaona ni bora wabadilishe na kumuimba Mourinho.

���� Gafla mbinu sina nimerudi kitaanee
��Nimeshindwa kuongoza timu nimesepa Chelsie
��umeneja umebaki jina hanitaki Romanee
��Hazard goli hakuna Costa ndo hataree
��wale shabiki zangu walonisifu kwa maneno mataamu
��leo ndo maadui zangu ni mitusi tu kwa instagram
��Fabi si mido wangu eti leo hanifahamu
��Hata matic nikimpigia anifokea kama zouma
��Na magazeti ya England kwa kukuza habari si unajuaga
��utasikia tafarani Mourinho wa Chelsie Amemwagwa
��Kwasasa nilivyomnyonge maneo ya kuwajibu sianaaaga
��Kama naiona michambo ya makocha wenzangu nliowachekaga
��Oh! nnayosema yana maana sababu hakuna anaejua kesho
��Anaepanga ni Rabana ila ameficha ni confidential
��Ukisali omba sana na anaekuja asiwe kichekesho mana rafiki wa jana ndo adui mkubwa keshooo.

Watumishi waliogushi Vyeti Wamkimbia Waziri wa Magufuli
Muhongo adai hataki kusikia kukatika kwa Umeme, afuta likizo Tanesco