Watumishi 219 waliobainika kugushi vyeti vilivyowawezesha kupata ajira serikalini wameripotiwa kukimbia vituo vyao vya kazi wakiukimbia mkono wa serikali ya awamu ya tano.

Watumishi hao walichukua hatua hiyo baada ya Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki kufanya ziara ya kushtukiza katika idara, vitengo vya ofisi ya rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na kubaini uwepo wa wafanyakazi hao waliogushi vyeti.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Rasilimali watu Utumishi, Leonard Mchau alisema kuwa ofisi hiyo imefanya uhakiki wa vyeti vya watumishi 704 na kubaini watumishi 219 waliotumia vyeti vya kugushi na  kwamba watumishi hao wamekimbia vituo vyao vya kazi baada ya kubainika.

Mheshimiwa Angela Kairuki (Picha kutoka Maktaba)

Mheshimiwa Angela Kairuki (Picha kutoka Maktaba)

Waziri Kairuki aliagiza kufanyika kwa zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wote wa serikali na kwamba watakaobainika walitumia vyeti vya kugushi waondolewe kwenye mfumo wa mishahara pamoja na kuchukuliwa hatua stahiki.

“Wasilisheni vyeti vyote baraza la mitihani kwa ajili ya uhakiki na baada ya uhakiki muwachukulie hatua stahiki watumishi wanaoonekana kutumia vyeti visivyo halali kwao,” alisema Kairuki.

Jerry Muro Kufikishwa Mbele Ya Kamati Ya Maadili
Wimbo Wa Diamond Watumika Kumtumia Salamu Jose Mourinho