Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameagiza watendaji wa shirika hilo kuhakikisha wanashughulikia upatikanaji wa umeme nchini kwani hataki kusikia tatizo la kukatika kwa umeme.

Profesa Muhongo aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya ukaguzi katika mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta Gas Plant.

Waziri huyo alitangaza kusitisha likizo za wafanyakazi wa shirika la umeme nchini (Tanesco) ili wajikite katika kushughulikia matatizo ya umeme ili suala la kukatika kwa umeme likome.

Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo alieleza kuwa bei ya umeme lazima ishushwe baada ya kuelezwa na Meneja Mohamed Kisiwa kuwa gharama za kuuza umeme huo kwa walaji ni mara mbili ya gharama za kuzalisha.

Meneja Mohamed alisema kuwa gharama za kuzalisha Unit moja ya umeme ni shilingi 90 na huuzwa kati ya shilingi 180 na 187.

“Utauzaje umeme mara mbili ya gharama za uzalishaji,  tunataka kuwapunguzia wananchi bei ya umeme  na kwenye mkutano wetu wa kesho (leo) tutajadili  kupunguza bei ya umeme..haya mahesabu hayajakaa sawa maana unazalisha uniti moja kwa Sh. 90 na kuuza kwa Sh. 180 tutajadiliana mpunguze,” alisema Muhongo.

Wimbo Wa Diamond Watumika Kumtumia Salamu Jose Mourinho
Lowassa awashinda wanasiasa 1000 Wakubwa duniani Kote