Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amewashinda wanasiasa wakubwa 1000 duniani kote walioshindanishwa na Kamati ya Maadili, Amani na Haki za binadamu katika kikao kilichofanyika nchini DRC Congo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mchungaji William Mwalanga aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa taasisi 1200 duniani zimempa Lowassa Tuzo ya Amani iliyokuwa inashindaniwa na wanasiasa hao.

Alisema kuwa wajumbe 1400 waliohudhuria wakitoka katika mataifa ya bara la Marekani, Asia, Ulaya na Afrika walimpigia kura Lowassa na kumuwezesha kushinda tuzo hiyo.

Alieleza kigezo kilichokuwa kikitumika ni kumpata kiongozi Bora wa amani wa mwaka 2015, ambaye anajali na kuangalia maslahi ya jamii badala ya madaraka.

Lowassa alichaguliwa baada ya kubainika kuwa alidumisha amani hata baada ya kushindwa uchaguzi wa urais uliokuwa na upinzani mkali Oktoba 25 mwaka huu.

 

Muhongo adai hataki kusikia kukatika kwa Umeme, afuta likizo Tanesco
Wanyarwanda Waidhinisha Uwezekano wa Kagame Kutawala hadi 2034