Wananchi nchini Rwanda wameonesha kuidhinisha kwa kishindo marekebisho ya katiba ya nchi hiyo itakayomruhusu rais Paul Kagame kuwania nafasi ya urais kwa mihula mingine mitatu.

Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo imeeleza kuwa katika matokeo ya awali yaliyokusanywa katika vituo 21 kati ya vituo 30 yanaonesha kuwa wananchi wameunga marekebisho ya katiba kwa asilimia 98.1 ya kura zote zilizohesabiwa.

“Tumeona matakwa ya wananchi, iko wazi kuwa wanachokitaka wananchi wa Rwanda watakifanikisha,” Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Kalisa Mbanda aliliambia gazeti la New Times la nchini humo.

Matokeo yote yanatarajiwa kutangazwa leo jioni huku ishara ya ushindi mkubwa ikionesha kumruhusu Kagame kuwania nafasi ya urais na huenda akawa rais wa nchi hiyo hadi mwaka 2034.

 

Lowassa awashinda wanasiasa 1000 Wakubwa duniani Kote
Justice Majabvi Kuchagua Mbivu Ama Mbichi Za Simba