Mapigano kati ya jeshi la DR Congo na waasi wa M23 yanaripotiwa kuendela kwa kasi wakati ambapo viongozi wa eneo hilo wakitoa wito wa kutafuta amani ya makundi yote yenye silaha kujiondoa katika eneo linalokaliwa kwa mabavu ifikapo Machi 30, 2023.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha usalama kilisema, mapigano yalianza saa kumi na moja asubuhi katika eneo la Kitshanga, kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa mashariki wa Goma.
Inaaminika kuwa zaidi ya makundi 120 yenye silaha na wanamgambo wa kujilinda wanapigana mashariki mwa DRC huku kundi la M23 likituhumu DRC kwa kupuuza ahadi ya kuwajumuisha wapiganaji wake katika jeshi.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, inaishutumu jirani yake Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi, mashtaka yanayoungwa mkono na kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa, ambayo Kigali inayakanusha.