Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara baina ya wapinzani wa jadi, Yanga na Simba uliopigwa katika uwanja wa Uhuru umemalizika kwa sare yakufungana bao 1-1.
Simba ndio waliotangulia kuata bao la kuongoza kupitia kwa Shiza Ramadhani Kichuya dakika ya 58 amablo hata hivyo halikudumu kwa muda mrefu kwani dakika ya 60 Obrey Chirwa aliipatia Yanga bao la kusawazisha.
Shiza Ramadhani Kichuya amefunga goli lake la tatu mfululizo dhidi ya Yanga kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara tangu asajiliwe na Simba msimu uliopita akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
-
Moto wa Man City hauzimiki, Liverpool, Arsenal nao kifua mbele
-
Anthony Martial aivunja Tottenham
-
Koeman aeleza sababu ya kutimuliwa Everton, amtaja Giroud
October 1, 2016 Kichuya aliifunga Yanga kwa mara ya kwanza akiwa Simba bao lake likiwa ni la kusawazisha wakati timu hizo zilipotoka sare ya kufungana 1-1 kwenye uwanja wa taifa.
February 25, 2017 Kichuya akaifunga tena Yanga kwa mara ya pili mfululizo kwenye mechi za ligi Simba ilipopata ushindi wa magoli 2-1 kwenye uwanja wa taifa na leo October 28, 2017 Kichuya ameweka rekodi ya kuifunga Yanga kwa mara ya tatu mfululizo kwenye mechi za VPL mechi iliyochezwa uwanja wa Uhuru.