Kiungo na nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure amesema bado hajakata tamaa ya kuitumikia klabu ya Man City, licha ya kuenguliwa kwenye kikosi kitakachoshiriki ligi ya mabingwa msimu wa 2016/17.

Toure ameonyesha ujasiri wa kutaka kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Etihad Stadium, wakati alipohojiwa na gazeti la Daily Mail la nchini England na kusema anajipanga kuwasilisha maombi ya kutaka asaini mkataba mpya.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33, amekua katika hali ya sintofahamu dhidi ya meneja mpya wa Man City Pep Guardiola, jambo ambalo limezua hofu ya wawili hao kutopika chungu kimoja tangu wakiwa FC Barcelona.

Mwanzoni mwa juma hili wakala wa Toure (Dimitri Seluk), alisema huenda mchezaji wake akasaka mbinu za kuihama Man City wakati wa majita ya baraji (mwezi Januari) kufutia mazingira yaliyomzunguuka huko Etihad Stadium tangu alipowasili Pep Guardiola.

Mpango huo wa wakala, unaonyesha kwenda tofauti na malengo ya Toure ambaye tayari amesisitiza kutokukata tamaa ya kuendelea kuitumikia Man City.

Ray Parlour Ampendekeza Diego Simeone Arsenal
Eddie Howe: Sio Wakati Sahihi Wa Kufikiria Ajira Ya Arsenal