Msanii mkongwe wa filamu Yusuph Mlela ambaye kwa sasa anafanya vizuri ndani ya tamthlia ya Kashfa inayorushwa na Azam TV, amewataka wasanii wenzake wa filamu kuamka na kuacha kulalamika na kufanya kazi kwa bidii.

Mlela anaamini kufanya kazi kwa bidii ndio njia pekee ya kujikomboa katika tasnia ya filamu, hivyo wasanii waache kusingizia soko la filamu kushuka.

Mlela amedai kuwa wasanii wengi wanakata tamaa kwa kauli ya soko limeyumba wakati wao ndiyo watu pekee ambao wanaweza kuikomboa tasnia ya filamu.

“Suala la soko wadau wanasema limeyumba, lakini naweza kusema huu ni wakati wa kuamka na kuanza kufanya kazi upya kulikomboa soko la filamu, kama wanasema kazi ni mbaya tufanye kazi nzuri, kila kitu tunaweza kufanya. Mimi nadhani huu ni wakati wa wasanii wa filamu kuamka na kufanya kazi kwa bidii ili kuirudisha ile hali ya zamani,” alisema Mlela.

Kwa sasa Yusuph Mlela anajipanga kuachia filamu yake mpya itakayojulikana kwa jina la ‘Mr Bodaboda’ Machi mwaka huu.

Nape awataka wadau wa michezo kushirikiana na Serikali
TMA yatoa tahadhari kuhusu hali ya hewa