Timu ya soka ya taifa ya Zanzibar maarufu kama Zanzibar Heroes mchana wa leo(Novemba 24,2015) imepoteza tena mchezo wake wa pili wa michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup baada ya kupokea kichapo kizito cha mabao 4-0 kutoka kwa Uganda.

Katika mhezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Awassa huko nchini Ethiopia, Zanzibar Heroes imeshuhudia wachezaji wake wawili wakilimwa kadi nyekundu.

Wachezaji hao ni golikipa Mwadini Ali(kadi dakika ya 14) na Mudathir Yahya(kadi dakika ya 75).

Mabao ya Uganda katika mchezo huo yamefungwa na Farouk Miya aliyefunga mabao mawili ya mwanzo katika dakika za 10 na 14 huku bao la tatu likifungwa na Erisa Ssekisambu(dakika ya 48) na la nne limefungwa na Denis Okoth (dakika ya 78)

Kupoteza mchezo hii leo kwa Zanzibar kumeiweka katika hali mbaya zaidi ya kufungasha virago kufuatia kushika mkia baada ya kupoteza pia mchezo wake wa awali dhidi ya Burundi kwa kufungwa 1-0.

CAF YAENDESHA SEMINA YA LESENI ZA VILABU
Wakata Miwa Waendelea Kujichua Kwa Ligi Kuu