Wavuvi watatu kati ya nane wa Wilaya ya Micheweni Pemba, waliokuwa wamepotea kwenye boti 2, wamepatikana wakiwa hai eneo la Watamu nchini Kenya huku mwenzao mmoja akihofiwa kufariki.

Kwamujibu wa taarifa zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Micheweni, Haji Khatibu amesema kuwa wavuvi waliopatikana ni Omar Ali Hassan (50), Kombo Ali Hassan (40), na Rashid Othman Ali (30), wote wakazi wa kijiji cha Shumba Micheweni.

Kwa upande wa ambao bado hawajaonekana na wala hakuna taarifa zao ni pamoja na Kombo Fakih Mwalimu (55), Mwalimu Bosi Faki (32), Said Ali Omar (50), na Omar Kombo Fakih (25), ambo walikuwa kwenye boti moja.

Aidha mbunge huyo, ameshauri wavuvi kuendelea kufuatilia kwa ukaribu taarifa za mamlaka ya hali ya hewa na wakihisi bahari imetangaziwa kuchafuka wasijaribu kwenda kazini.

Kwa upunde wa polisi mkoa wa kaskazini Pemba Shehan Mohamed Shehan, amesema awali hawakuwa na taarifa rasmi za kupotea kwa wavuvi hao, ingawa baada ya kuzipata walifika kijijini Shumba akiwa na kamati nzima ya ulinzi na usalama.

Kamanda Mohamed ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa rasmi zilitolewa boti nne kwa ajili ya kuwatafuta wavuvi hao.

Tukio hilo lilitokea baada ya upepo mkali uliotokea katika mji wa Mcheweni Pemba na kupelekea kupotea kwa boti mbili zilizokuwa na wavuvi nane.

 

Mpina atangaza kiama, 'Hata mkiniua atachaguliwa waziri mwingine'
Korea Kaskazini yarusha makombora ya masafa mafupi