Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewatangazia kiama wavuvi haramu waliohusika katika mauaji ya watu wanne, akiwemo ofisa mfawidhi wa rasilimali za uvuvi kanda ya Ukerewe yaliyotokea hivi karibuni.

Ameyasema hayo wakati akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa Ofisa Mfawidhi aliyeuawa katika mapambano kati ya wananchi na maofisa wa kikosi cha kupambana na uvuvi haramu wa kanda hiyo.

”Natangaza vita haramu, vita mpya na tutawasaka kila mahali, tutaimarisha sekta zote kuhakikisha uvuvi haramu unakomeshwa na hata mkiniua leo atateuliwa waziri mwingine, hamuwezi kupona kwa kutumia nguvu,” amesema Mpina.

Aidha, waliofariki katika mapambano hayo ni Ofisa Mfawidhi wa rasilimali za uvuvi kanda ya Ukerewe, Ibrahim Nyangali (38), na wakazi wa kisiwa hicho ambao ni,  Damian Joseph (18), Malanja Malima (18) na Chrisant Christian (47).

Hata hivyo, Waziri Mpina ameongeza kuwa wavuvi haramu hawawezi kushindana na Serikali na alitangaza kuanza oparesheni ya kuwasaka wavuvi haramu iliyoanza jana Julai 24.

JPM aagiza yafanyike marekebisho ya sheria ya TAZARA
Zanzibar: Wavuvi waliopotelea Baharini wapatikana Kenya wakiwa Hai