Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza mchakato wa kufanya marekebisho ya sheria ya TAZARA, ili kuwezesha kila nchi kuwekeza katika shirika hilo kwa lengo la kuboresha usafirishaji wa abiria na mizigo.

Ameyasema hayo leo Julai 25, alipopanda treni ya TAZARA kutoka Dar es salaam kuelekea Kisaki Mkoani Morogoro, ambapo amezungumza na viongozi wa TAZARA na kuwataka kuwasilisha mapendekezo yao, juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuboresha usafirishaji.

Reli ya TAZARA ina uwezo wa kusafirisha tani milioni 5 za mizigo kwa mwaka, lakini kutokana na uwekezaji mdogo kuna upungufu mkubwa wa Injini na Mabehewa na kupelekea kusafirisha mizigo chini ya tani laki 3 kwa mwaka.

Rais Magufuli ameongozana na mke wake Mama Janeth Magufuli, ambapo kesho Julai 26 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuweka jiwe la msingi, katika mradi wa uzalishaji wa umeme katika Mto Rufiji.

Rais wa Tunisia afariki dunia
Mpina atangaza kiama, 'Hata mkiniua atachaguliwa waziri mwingine'