Katika kuonyesha utekelezaji wa agizo lililotolewa na Tanesco la kutoa wiki mbili kwa wadaiwa sugu wa deni la umeme, Teyari Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imeanza kulipa deni inalodaiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), teyari Zanzibar imelipa jumla ya Sh. bilioni 10 kati ya sh bilioni 127.87 ambazo Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) linadaiwa  na Tanesco,

Hayo yamebainishwa katika mazungumzo yaliyofanyika jana kati ya Rais Dkt. John Magufuli na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu Jijini Dar es salaam.

Aidha, Mazungumzo hayo yalihudhuliwa pia na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Kahiwa Bishaija na Meneja Mwandamizi wa Fedha wa Shirika hilo, Sadock Mugendi.

Akizungumzia deni la Zanzibar, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa pamoja na kiasi hicho cha Sh bilioni 10 ambacho kilishalipwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kulipa deni hilo mpaka litakapomalizika.

Vile vile, Prof. Muhongo ametoa wito kwa wadaiwa wote sugu kulipa madeni yao katika kipindi cha siku tano zilizobakia kwakuwa wasipolipa watakatiwa Umeme kama ilivyoagizwa.

Hata hivyo, hivi karibuni Tanesco kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo aliwataja wadaiwa sugu wa hilo kuwa ni Wizara na Taasisi za Serikali zinazodaiwa  zaidi ya Sh  bilioni 52.53, huku Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) likidaiwa  bilioni 127.87 na Makampuni binafsi na wateja wadogo wadogo deni lao likiwa zaidi ya bilioni 94.97.

Mbowe atoa ya moyoni kuhusu Madaktari kupelekwa Kenya
Magazeti ya Tanzania leo Machi 20, 2016