Magwiji wa soka mjini Madrid, Hispania (Real Madrid FC) usiku wa kuamkia leo walitwaa ubingwa wa ligi ya nchi hiyo La Liga, kwa kuchabanga Villareal FC mabao mawili kwa moja.

Real Madrid wametwaa taji la 34 la La Liga, wakiongozwa na meneja wa Ufaransa Zinadine Zidane, wakicheza kwenye Uwanja wa Alfredo do Stefano.

Mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema alifungia klabu hiyo bao la kuongoza dakika ya 29 na la ushindi dakika ya 77 kwa mkwaju wa Penati huku lile la Villarreal likipachikwa na Vicente Iborra dakika ya 83.

Real Madrid imetwaa taji hilo ikiwa imeshinda jumla ya michezo kumi  mfululizo jambo linalowafurahisha mashabiki pamoja na benchi la ufundi la klabu hiyo.

Zidane amesema kuwa ilikuwa ni ngumu kufikia mafanikio jambo ambalo linampa furaha pamoja na wachezaji wake.

“Ligi ina jumla ya mechi 38 na ni ngumu kwangu kushinda ila kwa haya yaliyotokea ni ushindi mkubwa kwetu.” amesema.

Real Madrid imetwaa ubingwa ikiwa imebakiza mechi moja mkononi na ina pointi 86 ambazo hazitafikiwa na mpinzani wake Barcelona mwenye pointi 79 wote wakiwa wamecheza mechi 37.

Magari 25 yenye ving'ora na taa kali yakamatwa Dodoma
Usajili majira ya kiangazi watajwa England