Wakati Rais John Magufuli akiendelea na kazi yake ya kutumbua majibu na kuokoa fedha za umma pamoja na kurekebisha mishahara mizito ya vigogo, mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo) wameendelea kumuandama kuhusu kipato chake.

Zitto ambaye miaka miwili iliyopita alidai kuwa Rais alikuwa akipokea mshahara wa shilingi milioni 30 bila kukatwa kodi, amemtaka Rais Magufuli kutaja mshahara wake hadharani pamoja na makato yake ya kodi.

Hivi karibuni, Zitto aliwahi kudai kuwa Rais Magufuli ni mmoja kati ya watumishi wa umma ambao hawalipi kodi kupiti mishahara yao.

Akizungumzia kauli ya Rais Magufuli ya kupunguza mishahara ya vigogo wanaolipwa hadi shilingi milioni 40 hadi shilingi milini 15, Zitto alisifu hatua hiyo lakini alimtaka awe wa kwanza kutaja mshahara wake na kwamba akubali kuanza kukatwa kodi kama watumishi wengine.

“Ni vyema sasa akaweka wazi mshahara wake na akakubali ukatwe kodi ili iwe mfano kwa watumishi wengine na hata Tanzania iwe mfano wa kuigwa na nchi nyingine,” Zitto ananukuwaliwa.

Kadhalika, Tundu Lissu alirejea kauli ya Zitto huku akiongeza kuwa Rais na viongozi wengine wa ngazi za juu akiwemo Makamu wa Rais, Waziri Mkuu wanapaswa kuchukua hatua hiyo kama mfano kwa watumishi wengine.

Hata hivyo, Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angela Kairuki alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu suala la mshahara wa Rais alisema kuwa hayuko tayari kulizungumzia suala hilo.

Magufuli awajibu wapinzani, aweka wazi mshahara wake
Wakala Wa Romelo Lukaku Afichua Siri Nzito