Baada ya wadau wa siasa na baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani kumtaka Rais Magufuli kuanika hadharani mshahara wake pamoja na makato ya kodi, amechukua hatua hiyo.

Rais Magufuli ametoa majibu ya mshahara wake leo kupitia kipindi cha Clouds360 cha Clouds TV baada ya kusikiliza magazeti yaliyokuwa yakisomwa na watangazaji wa kipindi hicho huku maandishi yakiwa na matakwa ya kujua mshahara wa kiongozi huyo mkuu wa nchi.

Dk. Magufuli alisema kuwa yeye hupokea kiasi cha shilingi milioni tisa na laki tano (9,500,000) huku akiahidi kutoa nyaraka za malipo ya mshahara wake punde atakapotoka mapumzikoni nyumbani kwake Chato.

Hivi karibuni, Dk. Magufuli ameahidi kupunguza mishahara ya baadhi ya vigogo inayozidi shilingi milioni 15 ili mtumishi anayepata mshahara mkubwa zaidi usizidi kiasi hicho.

Katika serikali ya awamu ya nne iliyokuwa chini ya utawala wa Dk. Jakaya Kikwete, Zitto Kabwe na baadhi ya wabunge wa upinzani walikuwa wakitaja mshahara wa Rais kuwa ni zaidi ya shilingi milioni 30. Hata hivyo, Ikulu ilikuwa ikikanusha taarifa hizo ingawa haikutaja mshahara halisi.

Malinzi: Sitashangaa Hata Kesho Uwanja Wa Karume Nao Ukipigwa Mnada
Zitto, Lissu wang’ang’ana na Magufuli