Mshambuliaji wa Man Utd Zlatan Ibrahimovic atakosa michezo mitatu ijayo ya klabu hiyo, kufuatia kukubali makosa ya utovu wa nidhamu aliyoyafanya wakati wa mchezo wa ligi ya England mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya AFC Bournemouth.

Zlatan amekubali kufanya kosa la kumpiga kiwiko beki wa AFC Bournemouth Tyrone Mings, kitendo ambacho kilitokea dakika chache baada ya kukanyagwa kichwani na beki huyo.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35 atakosa mchezo wa hatua ya robo fainali ya kombe la FA dhidi ya Chelsea utakaochezwa mwanzoni mwa juma lijalo dhidi ya Chelsea, kisha mchezo wa ligi wa Machi 13 dhidi ya Middlesbrough na mwingine dhidi ya West Brom utakaochezwa Aprili mosi.

Zlatan atarudi uwanjani Aprili 04 baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungiwa michezo mitatu, na siku hiyo Man Utd watapambana na Everton kwenye uwanja wa Old Trafford.

Hata hivyo Zlatan atakuwa sehemu ya kikosi cha Man Utd kesho ambacho kitacheza mchezo wa Europa league dhidi ya FC Rostov, kutokana na mchezo huo kutokua chini ya himaya ya chama cha soka nchini England.

Kwa upande wa Tyrone Mings anasubiri hukumu kutoka FA, baada ya kukana mashtaka kwa kuwasilisha utetezi ambao anaamini utamsaidia katika kesi hiyo.

Mings amedai kuwa, hakukusudia kumkanyaga kichwani Zlatan, bali alijikuta akifanya hivyo baada ya kujitahidi kuukwepa mkono wa mshambuliaji huyo ili asiukanyage.

Video: Ni ruksa kuikosoa Serikali - Nape, Wateule wa Rais, Wabunge wanavyotunishiana misuli
Wenger Amtupia Lawama Mwamuzi