Bara la Afrika litapata faida ya kuwa na timu mbili zaidi miongoni mwa timu shiriki za fainli za kombe la dunia, kuanzia mwaka 2026 kufuatia azimio la rais mpya wa shirikisho la soka duniani FIFA, Gianni Infantino ambalo ataliwasilisha katika mkutano mkuu.

Infantino, alisisitiza dhamira hiyo alipozungumza na waandishi wa habari nchini Nigeria mara baada ya kuwasili mjini Abuja hapo jana, ambapo alisema kuna haja ya timu za Afrika kuongwezwa kutoka idadi ya timu tano hadi saba, ikiwa ni sehemu ya mipango ya kutaka kuongeza timu kutoka 32 hadi 40.

Kuongeza idadi ya timu shiriki katika fainali za kombe la dunia, ilikua ni moja ya sera za Infantino wakati alipokua akisaka kura za urais kwa wajumbe wa shirikisho la soka duniani FIFA, kabla ya kuchaguliwa miezi kadhaa iliyopita.

“Ninaamini katika fainali za mwaka 2026, timu shiriki zitaongezeka kutoka 32 hadi 40, inatulazimu kuheshimu fainali za mwaka 2018 na 2022 ambazo tarayi zimeshaandaliwa na haitowezekana kufanya mabadiliko hayo,”

“Hii ilikua ni moja ya sera zangu wakati nafanya kampeni za kuwania nafasi ya urais wa FIFA, sina budi kutimiza kwa vitendo kwa kuwashawishi wajumbe wa mkutano mkuu ili waweze kulipitisha jambo hili na lianze kufanyiwa kazi katika faianli za mwaka 2026.” alisema rais wa FIFA.

Afrika imekua ikiwakilishwa na timu tano katika fainali za kombe la dunia tangu mwaka 1998, na ilipata bahati ya kuwakilishwa na timu sita katika fainali za mwaka 2010 zilizofanyika Afrika kusini, ambapo Bafana Bafana waliingia kama wenyeji.

Azimio la Infantino la kuongeza timu kutoka 32 hadi 40, pia litayanuifaisha mabara mengine kuongeza timu shiriki, ambapo tayari Afrika imeshathibitishiwa kuwa na faida ya timu mbili zaidi.

Bordeuax Waridhishwa Na Kiwango Cha Mathieu Debuchy
Avamia kituo cha wenye ulemavu na kuua 19 kwa kisu