Mwanamuziki kutoka Oukland Calfornia nchini Marekani, Alexander Edwards maarufu Alexander ‘A.E’ ameonyesha kujutia kitendo cha kumsaliti mzazi mwenzie mwanamitindo maarufu Duniani Amber Rose.

Ni kwa kile kinachodaiwa kuwa Alexander akiwa kwenye mahusiano na Amber aliwahi kumsaliti kwa kuwa na mahusiano ya nje na wanawake wasiopungua 12, licha ya kuwa ndani ya mahusiano na mrembo huyo.

Alexander ameonyesha kujutia makosa hayo na kudhihirisha kuwa anahitaji kurudiana na mzazi mwenzie, Amber Rose.

Rapa huyo ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kumuomba msamaha Amber Rose na kuweka wazi kuwa anahitaji mahusiano yao yarudi kama zamani kwa kua kuachana kwao kumeharibu sehemu muhimu ya maisha yake.

“Kwa unyenyekevu ninataka kuomba radhi kwa mke wangu mrembo Amber Rose, ukweli ni kuwa hukustahili nilichokifanya kwako.
Wewe ni mtu mwema sana na mzazi bora kwa watoto wetu, nisamehe kwa maumivu niliyo kusababishia, mtoto wangu Slash na mtoto wangu wa kambo, Sebastian.” Aliandika Alexander.

Licha ya kuandika hayo aliendelea kuweka wazi kuwa yuko tayari kufanya jambo la namna yeyote ili kurejesha uhusiano wake na Amber kwenye hali ya usawa.

Ambapo kupitia kwenye Insta story yake aliandika ujumbe mwingine mfupi uliosomeka. “Ninachotaka ni kuhakikisha nairudisha familia yangu, na hakika niko tayari kufanya jambo lolote ili kurejesha kila kitu kwenye hali yake, Tafadhali naomba nisamehe.” Aliongeza.

Kwa mujibu wa The Source, mnamo Agosti 2021, Mwanamitindo Amber Rose alimshutumu Alexander kufanya vitendo vya vichafu na kumsalitia kwa kutoka kimapenzi na takribani wanawake 12.

Na hapo ndipo Kasheshe iliyopelekea kutengana kwao ilipoanzia.

Uzinduzi shule ya Msingi Museveni-Chato
Kirusu kipya cha Corona chafunga mipaka