Serikali ya Sri Lanka, inakabiliana na baadhi ya viongozi wa waandamanaji walioandaa vuguvugu lililomwondoa madarakani rais wa nchi hiyo mwezi uliopita, huku ikiwakamata raia watatu akiwemo aliyeiba kikombe cha kunywea bia na aliyekalia kiti cha Rais.

Katika mpango huo, tayari Wanaharakati wakuu wamekamatwa, akiwemo Joseph Stalin, kiongozi wa chama cha walimu, na Mahanama Thero, mtawa wa Kibudha huku wengine wakipigwa marufuku ya kusafiri huku Serikali ikiamuru kuondolewa kwa mahema ya mwisho ya maandamano yaliyosalia.

Mwanaharakati na kamishna wa zamani wa haki za binadamu nchini Sri Lanka, Ambika Satkunanathan amesema Serikali ilikuwa ikiwawinda watu kwa makosa madogo ili kukomesha upinzani.

Waliokamatwa ni pamoja na muandamanaji anayedaiwa kuiba bendera rasmi ya rais, mwingine anayeshtakiwa kwa kuiba kikombe chake cha bia, na watatu ambaye anayesemekana alikalia kiti chake.

Rais mpya wa nchi hiyo, Ranil Wickremesinghe aliwaita baadhi ya waandamanaji kuwa ni tishio la “fashisti” mara tu alipoingia madarakani, na kusema mamlaka itachukua hatua dhidi ya wale ambao walikuwa wamevamia majengo ya serikali.

Mara baada ya kuchukua madaraka, Rais Wickremesinghe aliwatuma polisi kufanya uvamizi mkali wa alfajiri kwenye tovuti ya maandamano, ambapo Wanaharakati wakisema uvamizi huo unaotokana na maelekezo ya Rais unalenga kuwatunishia misuli na kujaribu kuwaadhibu wapinzani.

TAMWA yataka marekebisho katiba vyama vya siasa
Sita wakamatwa ulaghai wa tovuti mapenzi ya jinsia moja