Meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte, bado anaendelea na mpango wa kutaka kumsajili beki wa kati wa klabu bingwa nchini Italia Juventus FC Leonardo Bonucci.

Conte alishindwa kukamilisha mpango wa kumsajili beki huyo kisiki, wakati wa majira ya kiangazi, lakini katika kipindi hiki cha kuelekea mwezi Januari ameonyesha dhamira nyingine kwa Bonucci, ambaye aliwahi kufanya nae kazi kwa mafanikio makubwa mjini Turin.

Harakati za kuiwania saini ya Bonucci, zimekuja kutokana na uwezekano wa beki na nahodha wa Chelsea John Terry kuwa kwenye mipango ya kutaka kuondoka Stamford Bridge na kutimkia mashariki ya mbali (China) ama nchini Marekani.

Hata hivyo Conte ameweka mpango namba mbili wa kumsajili beki wa kati wa AS Roma Antonio Rudiger ama Michael Keane wa Burnley endapo atashindwa kufanikisha kuvunja mkataba wa Bonucci.

Video: Mfumuko wa bei wazidi kushuka nchini
Safari Za Timu Zote Za Taifa