Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Uholanzi Arjen Robben amekamilisha mpango wa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia FC Bayern Munich.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea na Real Madrid amekubali kufanya utaratibu huo, ambao utamuwezesha kusalia nchini Ujerumani akiwa na mabingwa hao hadi mwezi Juni mwaka 2018.

Robben mwenye umri wa miaka 32, aliwasili Allianz Arena mwaka 2009 na tayari amekuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa ligi ya nchini Ujerimani (Bundesliga) mara tano, kombe la chama cha soka nchini Ujerumani (DFB-Pokals) mara nne na ubingwa wa Ulaya (UEFA Champions League) mara moja.

“Ninafuraha ya kuendelea kubaki hapa, naamini nitafanya jitihada za kuendelea kuisaidia FC Bayermn Munich kwa kushirikiana na wenzangu, kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja,” Alisema Arjen Robben .

Kwa msimu huu, Robben tayari ameshafunga mabao sita katika michezo 14 aliyocheza chini ya utawala wa Carlo Ancelotti.

Hali Bado Ngumu Kwa Dimitri Payet
Mwijage atoa neno Tantrade kuhusu kasi ya viwanda